Tuesday, October 11, 2016

Vidonda vya tumbo

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo. Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kama Helicobacter pylori. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-inflamatory Drugs kama Aspirin au Diclofenachuweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu. Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum. 💢Makundi ya PUD Kuna makundi makuu yafuatayo ya ugonjwa huu 1. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo(Gastric ulcers) 2. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers) 3. Vidonda vinavyotokea kwenye koo(Oesophageal ulcers) 4. Vidonda vijulikanavyo kama Merckel’s Diverticulum ulcers. 💢Visababishi vya PUD Vidonda vya tumbo husababishwa na 🔴Maambukizi ya bakteria aina yaHelicobacter pylori: Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yeyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 yaduodenal ulcers. Hali hii husababishwa zaidi na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili. Matokeo ya kushindwa huku husababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis), uambukizi ambao huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali. Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Parietal cells.Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wagastrin pia uharibika, na hivyo kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo. 🔴Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs:Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaaniprostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo. 🔴Uvutaji wa sigara: Uvutaji sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike tu kuwa uvutaji sigara pekee hausababishi vidonda vya tumbo. 🔴Vyakula au viungo vya chakula vyenye uchachu: Kinyume na dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama vile pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo. 🔴Watu walio katika kundi la damu la O:Imeonekana pia kwamba kundi la damu lijulikanalo kama blood group O, halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo. 🔴Unywaji wa pombe: Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. 🔴Vitu vingine: Vitu vinavyohusishwa na uongezaji wa madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na upasuaji wa tumbo(major abdominal surgeries), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo; na kubadilishwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini. 💢Dalili au viashiria vya PUD Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula. Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula. Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara.Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua.Kichefuchefu na kutapikaKupoteza hamu ya kula na kupungua uzitoKutapika damuKupata haja kubwa cha rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbaliUwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa za kupunguza maumivu (NSAIDs) kwa muda muda mrefu bila kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo. 🌟SULUHISHO KWA KUTUMIA VIRUTUBISHO VYA KIADA.🌟 🔶1) Aloe vera jel Hichi ni kinywaji kilochotengenezwa na mmea wa aloe vera na kama inavyofahamika, aloe vera inauwezo wa kutibu vidonda tofauti ikiwemo vidonda vya tumbo. Na kila aliyetumia ameleta majibu mazuri ya kuondoa kabisa vidonda vya tumbo. Inamanufaa mengi, manufaa mengine nimeongelea kwenye mada ya "Moyo". 🔶2) Bee Propolis Hii imetengenezwa na nta inayotolewa na nyuki wa asali, nta hii hutumika kukinga mzinga na bacteria wanaoweza kudhuru mzinga. Lakini pia nta hii ni muhimu sana katika miili ya binadamu. Manufaa hayo ni, 🔵ina ongeza kinga ya mwili 🔵ina saidia kuuwa bacteria hatarishi kwenye mfumo wa chakula. 🔵 Huondoa uchovu wa akili 🔵 inaongeza uwezo wa kupona 🔵 inapunguza mikonyanzi 🔵 inahusika na kutatua allergies.

Wednesday, October 5, 2016

Mwalimu wa Saikolojia....

Mmmh najua hii italeta sekeseke, ila ningependa kila mmoja atoe maoni yake. Nini msimamo wake kama ingetokea hali hii, soma story hii na andika maoni yako tu. Siku moja katika darasa la jioni la watu wazima, mwalimu wa saikolojia aliingia darasani na kuwaambia wanafunzi; "Nataka tucheze mchezo, mtu yeyote yule naomba ajitolee aje hapa mbele" Mwanamke aitwae Cathy akatoka mbele. Mwalimu akamwambia aandike majina 30 ubaoni ya watu ambao anadhani ni wa muhimu katika maisha yake. Cathy akaandika majina ya wanafamilia yake yaani mumewe na mwanae, ndugu, majirani na marafiki zake. Mwalimu akamwambia Cathy afute majina matatu ambayo anadhani kwake sio ya muhimu sana kuzidi mengine. Cathy akafuta majina ya marafiki zake watatu. Mwalimu akamwambia Cathy afute tena majina matano zaidi, Cathy akafuta majina ya majirani zake watano. Hii iliendelea mpaka alipobakiwa na idadi ya watu wanne tu katika ubao. Haya yalikuwa majina ya wazazi wake, mumewe na mtoto wake wa pekee. Darasa zima wakabaki kimya, baada ya kugundua kuwa huu sio mchezo wa Cathy peke yake sasa. Mwalimu akamwambia Cathy afute majina mengine mawili kati ya yale manne yaliyobaki. Ulikuwa uamuzi mgumu mno kwa Cathy. Bila hiyari akafuta majina ya wazazi wake. "Futa jingine zaidi tafadhali" mwalimu alimwambia. Cathy akaishiwa pozi, na huku mikono ikimtetemeka na machozi katika macho yake akafuta jina la mwanae wa pekee. Na kubakiza jina la mume wake, Cathy alilia mno!!! Mwalimu akamwambia Cathy aende akakae. Baada ya muda kidogo mwalimu akamuuliza Cathy "kwanini mume wako? Wazazi wako ndio waliokulea na kukuza, Mtoto wako ndio huyo tu mmoja uliyenae!! Na unaweza ukapata mume mwingine!!! Kwanini??" Darasa likawa na ukimya wa hali ya juu, kila mmoja akitamani asikie ni nini Cathy atajibu. Cathy kwa ujasiri na utulivu akainuka na kusema, "siku moja wazazi wangu watatangulia kufariki (Mwenyezi Mungu anisamehe), mtoto wangu pia ataondoka pale atakapokua mkubwa kwenda kuanzisha familia yake. Mtu nitakayebaki nae kumaliza nae maisha hasa uzeeni ni mume wangu tu!! Yeye ndiye niliyeunganishwa nae na Mungu, mimi na yeye ni mwili mmoja." Wanafunzi wote wakasimama na kumpigia makofi kwa kushare nao ukweli na msimamo wa maisha yake. Huu ulikuwa uamuzi wa Cathy, yeye kwa mtizamo wake alimchagua mumewe. Je wewe ungechagua nani? Majibu yako tafadhali huku ukitaja na sababu!! Share na wengine waje na majibu yao hapa

Asili ya Coca-cola

Asili ya Coca-Cola Coca-Cola ni moja ya kampuni maarufu duniani, ambayo hutengenezwa soda maarufu ya Coke na vinywaji vingine vya soda. Lakini, ilikuwaje hadi ikawa na jina hilo? Labda umewahi kusikia kwamba Coca-Cola wakati mmoja ilikuwa na kiungo cha kusisimua ambacho kiliwafanya wateja kulipenda sana. Hii ni moja ya vilivyochangia jina lake. "Coca", kwa Kiswahili koka, ni jina la jani la mmea wa koka, moja ya viungo ambavyo mvumbuzi wa kinywaji hicho, mwanakemia wa Atlanta John Stith Pemberton, alichanganya na shira kutengeneza kinywaji chake. Majani ya koka hutumiwa kutengeneza kokeini. Wakati huo, mwishoni mwa karne ya 19, ilikuwa kawaida kwa majani ya koka kuchanganywa na divai na kuwa kinywaji cha kuchangamsha mwili. Kokeini yagundulika kwenye kiwanda cha Coca-Cola Kinywaji kipya alichotengeneza Pemberton kilikuwa njia nzuri ya kukwepa sheria zilizoharamisha uuzwaji wa pombe. Sehemu hiyo nyingine ya jina Coca-Cola inatokana na kiungo kingine chenye nguvu, ingawa si maarufu sana. Kiungo hiki ni kola. Kola asili yake ni Afrika Magharibi Ganda ambalo huwa na kokwa za kola ndani yake huwa na urefu wa inchi mbili na kabla ya kukauka, huwa za rangi ya kijani. Ndani yake huwa na sehemu yenye fundo za rangi nyekundu au nyeupe kabla hazijakauka. Asili ya kola ni Afrika Magharibi na zimekuwa zikitafunwa kwa miaka mingi na wenyeji kama kitu cha kuchangamsha mwili. Kokwa hicho huwa na kafeini na theobromine, ambavyo hupatikana pia kwenye chai, kahawa na kakao. Zina pia sukari na kolanin, ambayo huaminika kuwa kichangamsha moyo. Kufikia karne ya 19, kola zilianza kusafirishwa Ulaya na Marekani na zikaanza kutumiwa katika tembe zilizokusudiwa kutumiwa kuongeza nguvu mwilini. Papa Leo XIII Muda si muda, zilianza kutumiwa kwenye vinywaji. Kinywaji kimoja maarufu kilikuwa Vin Mariani, cha Ufaransa kilichotayarishwa kwa kuchanganya maji ya coca na divai nyekundu. Kilitengenezwa na mwanakemia Mfaransa Angelo Mariani, mwaka 1863, na Papa Leo XIII alikuwa mmoja wa waliokipenda sana. Malkia Victoria wa Uingereza, Thomas Edison, na Arthur Conan Doyle pia walikipenda sana. Kola zilidhaminiwa sana Afrika Magharibi Pemberton, naye alijitokeza na mchanganyiko wake akifuata mtindo huu lakini yeye hakutumia divai bali alitumia shira. Baada ya muda kokeini iliacha kutumiwa kwenye vinywaji, baada ya kutambuliwa kama dawa ya kulevya lakini kola ziliendelea kuwa maarufu. Kwa sasa, viungo pamoja na utaratibu wa kutayarisha soda za Coca-Cola huwa siri kuu, lakini taarifa husema huwa kola hazitumiwi tena. Badala yake, kampuni hiyo hutumia kemikali kuunda ladha sawa na ya kola. Hata hivyo, jina halijabadilika PICHA YA KWANZA NI MMEA WA COCA PICHA YA PILI NI MMEA WA COLA
HAYA NDIO MAAJABU YA ZAMBIA NA MALAWI. 1. Nchi zote Malawi na Zambia zilipata uhuru mwaka 1964 na zote hutumia pesa aina ya Kwacha. Marais wake wote, Dk. Kamuzu Banda (Malawi) na Dk. Kenneth Kaunda (Zambia) walizitumikia nchi zao katika nafasi za urais kwa muda mrefu na asili zao zinatatanisha, hawaeleweki kama ni Wamalawi na Zambia. Wote Kamuzu na Kaunda walikuwa na kaulimbiu inayofanana ya “Wamuyaya” (Life) ikiwa na ishara ya mamlaka. 2. Bakili Muluzi, alizaliwa 1943, ndiye aliyechukua madaraka kutoka kwa Kamuzu Banda. Fredrick Chiluba, alizaliwa 1943, ndiye aliyechukua madaraka kutoka kwa Kenneth Kaunda, na wote wawili Muluzi na Chiluba walifanya jaribio la kutaka kubadili Katiba ili wapate kipindi cha tatu cha uongozi lakini walishindwa. Wote Muluzi na Chiluba waliwataliki wake zao kwa sababu ya kukosekana uaminifu kwenye ndoa. 3. Wote, Muluzi na Chiluba waliwapeleka watangulizi wao mahakamani (Dk. Banda na Dk. Kaunda). 4. Bakili Muluzi alimpendekeza Bingu wa Mutharika kuchukua nafasi yake, wakati Frederick Chiluba alimpendekeza Levy Mwanawasa kuchukua nafasi yake na wote waliwafanyia kampeni wakati wa uchaguzi. 5. Wote Mutharika na Mwanawasa walishinda uchaguzi na kuwa marais wa tatu katika nchi zao. 6. Muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa marais, wote Mutharika na Mwanawasa walishindwa kuwabeba (kuwavumilia) watangulizi wao Muluzi na Chiluba. Wote wawili, Mutharika na Mwanawasa waliwapeleka watangulizi wao (Muluzi na Chiluba) mahakamani kwa makosa ya kujihusisha na rushwa. Sasa inavutia zaidi; Muluzi alishtakiwa na utawala wa Mutharika. Chiluba alishtakiwa na utawala wa Mwanawasa. 7. Bingu wa Mutharika alishinda kipindi cha pili cha uongozi, Mwanawasa alishinda kipindi cha pili cha uongozi. Mutharika alimchagua Joyce Banda kama Makamu wake wa Rais. Mwanawasa alimchagua Rupiah Banda kama Makamu wake wa Rais. 8. Mutharika alifariki akiwa madarakani katika kipindi chake cha pili kwa matatizo ya moyo (Cardiac Arrest). Mwanawasa pia alifariki akiwa madarakani katika kipindi chake cha pili kwa matatizo ya moyo (Cardiac Arrest). 9. Joyce Banda alichukua madaraka kutoka kwa Bingu wa Mutharika kutokana na kifo hicho. Rupiah Banda alichukua madaraka kutoka kwa Levy Mwanawasa kutokana na kifo hicho. Marais wote hawa waliochukua madaraka kutoka kwa marehemu waliitwa “Banda”! 10. Baada ya miaka 3, Rais Banda wa Zambia alishindwa kwenye uchaguzi na mpinzani wake Michael Sata. Banda wa Malawi naye ameshindwa kutetea i wake Peter

Tuesday, October 4, 2016

Maajabu ya Malawi na Zambia

HAYA NDIO MAAJABU YA ZAMBIA NA MALAWI. 1. Nchi zote Malawi na Zambia zilipata uhuru mwaka 1964 na zote hutumia pesa aina ya Kwacha. Marais wake wote, Dk. Kamuzu Banda (Malawi) na Dk. Kenneth Kaunda (Zambia) walizitumikia nchi zao katika nafasi za urais kwa muda mrefu na asili zao zinatatanisha, hawaeleweki kama ni Wamalawi na Zambia. Wote Kamuzu na Kaunda walikuwa na kaulimbiu inayofanana ya “Wamuyaya” (Life) ikiwa na ishara ya mamlaka. 2. Bakili Muluzi, alizaliwa 1943, ndiye aliyechukua madaraka kutoka kwa Kamuzu Banda. Fredrick Chiluba, alizaliwa 1943, ndiye aliyechukua madaraka kutoka kwa Kenneth Kaunda, na wote wawili Muluzi na Chiluba walifanya jaribio la kutaka kubadili Katiba ili wapate kipindi cha tatu cha uongozi lakini walishindwa. Wote Muluzi na Chiluba waliwataliki wake zao kwa sababu ya kukosekana uaminifu kwenye ndoa. 3. Wote, Muluzi na Chiluba waliwapeleka watangulizi wao mahakamani (Dk. Banda na Dk. Kaunda). 4. Bakili Muluzi alimpendekeza Bingu wa Mutharika kuchukua nafasi yake, wakati Frederick Chiluba alimpendekeza Levy Mwanawasa kuchukua nafasi yake na wote waliwafanyia kampeni wakati wa uchaguzi. 5. Wote Mutharika na Mwanawasa walishinda uchaguzi na kuwa marais wa tatu katika nchi zao. 6. Muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa marais, wote Mutharika na Mwanawasa walishindwa kuwabeba (kuwavumilia) watangulizi wao Muluzi na Chiluba. Wote wawili, Mutharika na Mwanawasa waliwapeleka watangulizi wao (Muluzi na Chiluba) mahakamani kwa makosa ya kujihusisha na rushwa. Sasa inavutia zaidi; Muluzi alishtakiwa na utawala wa Mutharika. Chiluba alishtakiwa na utawala wa Mwanawasa. 7. Bingu wa Mutharika alishinda kipindi cha pili cha uongozi, Mwanawasa alishinda kipindi cha pili cha uongozi. Mutharika alimchagua Joyce Banda kama Makamu wake wa Rais. Mwanawasa alimchagua Rupiah Banda kama Makamu wake wa Rais. 8. Mutharika alifariki akiwa madarakani katika kipindi chake cha pili kwa matatizo ya moyo (Cardiac Arrest). Mwanawasa pia alifariki akiwa madarakani katika kipindi chake cha pili kwa matatizo ya moyo (Cardiac Arrest). 9. Joyce Banda alichukua madaraka kutoka kwa Bingu wa Mutharika kutokana na kifo hicho. Rupiah Banda alichukua madaraka kutoka kwa Levy Mwanawasa kutokana na kifo hicho. Marais wote hawa waliochukua madaraka kutoka kwa marehemu waliitwa “Banda”! 10. Baada ya miaka 3, Rais Banda wa Zambia alishindwa kwenye uchaguzi na mpinzani wake Michael Sata. Banda wa Malawi naye ameshindwa kutetea kiti chake na mpinzani wake Peter Mutharika.

Kwa wale wakubet ( Betting)

Watu wengi katika ulimwengu wa GAMBLING wanajikuta wakipoteza kiasi kikubwa cha pesa bila hata ya kujitambua.Ni kutokana na kutokujua au kutambua misingi kadhaa ya kushiriki katika Mchezo huu LEO NAOMBA NIWAJULISHE WADAU WA MCHEZO JINSI AU NAMNA YA KUSHIRIKI KIKAMILIFU NA KUFANIKIWA KUSHINDA KWA KIASI KIKUBWA. KWA KUZINGATIA MAMBO HAYA #8 ,UTAWEZA KUFANIKIWA KUTENGENEZA FAIDA KUBWA KATIKA MCHEZO HUU. #1 . UFANYE UWE MCHEZO,KISIWE CHANZO CHA MAPATO. Watu wengi hufanya mchezo wa football betting kama ni kituo cha kujipatia mapato kwa ajili ya kukidhi haya mbalimbali za kimaisha kama vile 1.kulipa kodi ya nyumba, 2.Kupata ada ya watoto, 3.Kupata fedha ya kununua mali fulani i.e Pikipiki, Simu. 4. Kupata fedha ya kulipa Deni. ...na mengineyo! Hili ni kosa kubwa sana. Unapofanya huu mchezo kama ni chanzo cha pesa kwa ajili ya suala fulani, linakupotezea nafasi ya kuweza kufanya machaguzi ya Odds yaliyo sahihi.Watu wenye utaratibu huu ,huwa wanachagua Odds ambazo zitawaletea zao kubwa la pesa na kusahau kuwa si michezo yote katika orodha inayoweza kukupa tokeo chanya. (Kumbuka, Mahesabu ya kina hufanywa na wenye hizi Betting Companies kuhakikisha hakuna mtu anaweza kupata kiasi kikubwa cha pesa kama matokeo ya betting(Mkeka) wake). #2 . ZITAMBUE LIGI VIZURI. Watu wengi hujihisisha katika huu mchezo hata bila ya kutambia mienendo (Trend) ya ligi kuu mbalimbali barani Ulaya.Kutokana na Betting Companies kuwa na aina mbali mbali za "kubet", Pia kuna baadhi ya ligi zina "facilatate successful betting" kutokana na aina ya betting. Kwa mfano:- Ligi ya Uingereza(EPL) , inafaa sana kutumika katika kubeti katika category ya "NORMAL" kwa asilimia 80%.Hii ni kutokana na ligi kuwa na wababe wanaotabirika , Baadhi ya timu kuwa out-of-form kwa muda mrefu, Mjeruhi ya mara kwa mara. Ligi ya Spain(LA LIGA), inafaa sana kutumika katika "NORMAL" kwa silimia 70% na "HANDCAP" kwa silimia 30%( timu za R.madrid,Barca,A.madrid) Ligi ya Ufaransa(LIGUE 1).Kutokana na hii ligi kuto kuwa na wababe wa kueleweka , hapa ni mahali salama sana kuitumia "HANDCAP" 80% na.Pia ni ligi iliyo na idadi ndogo sana ya magoli hivyo basi "FOURTYFIVE" prediction inafaa.Hii ni kutokana na matokeo mengi ya ligi hii kuwa na tofauti ya goli moja. Ligi kuu ya Itali (Serie A), hii ligi haina tofauti sana na ligi kuu ya Ufaransa.Baadhi ya mechi huwa na tofauti ya goli moja, na mara nyingi huwa na matokeo ya suluhu katika dakika 45 za kwanza. Hivyo "HANDCAP" ina asilimia 60% na "FOURTYFIVE" ina asilimia 40%.(Tahadhari: Hii ligi inahitaji uchambuzi wa kina katika mechi zake kabla ya kuweka bet,) #3 . BOBEA KWENYE LIGI CHACHE TU. Si mbaya sana ukichagua baadhi ya timu zenye nguvu kutoka ligi nyingine, bali umuhimu wa kubobea katika ligi chache ni veyma zaidi.Hii itakufanya uwe mwenye uelewa na utambuzi wa kutosha na mwenendo wa hizo ligi chache. Pia hii itakuwezesha kuweza kufanya maamuzi sahihi yaliyo na ufahamu na uelewa yakinifu., #4 . MARA NYINGI NI VYEMA KUFUATA HISIA. Umeshawahi kutazama orodha ya michezo/mechi za siku husika kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho, na katika akili yako kuna hisia/vochochezi ambavyo vina kuambia kwamba "huyu anashinda" au "huyu anafungwa" au "hii mechi suluhu"? Basi kwa taarifa yako, hizo hisia-za-mwazo(PRESCIENCE) husadikika kuwa sahihi kwa asilimia 80%. Hii ni kwa upande wa wale wanao-Bet katika category ya "NORMAL". #5 . EPUKA USHABIKI. Kuna nyakati ambazo inakuhitaji uchague mechi ambayo timu uipendayo inacheza.Hiki kimekuwa kipindi kigumu sana kwa watu wengi.Hupenda kuchagua timu zao kuwa zitashinda hata kama ukweli ni kwamba zinauwezekano mkubwa sana wa kupoteza mchezo. Au kuwekea timu fulani ishindwe kwa mategemeo timu yake(anayoishabikia) iendelee kuongoza ligi. Ukiona umejawa na hisia za ushabiki na huwezi shindana nazo, basi ni bora kuacha kabisa kuchagua mechi hizo. #6 . FANYA UCHAMBUZI YAKINIFU. Hili ni pamoja na kuzingatia aina ya mchezo unaocheza. Mfano -NORMAL; katika hii category unashauriwa kuchagua mechi zenye timu dhaifu na imara.Hii inaleta uwezekano wa kutokea kwa matokeo yaliyo-tabiriwa. -HANDCAP; hapa unashauriwa kuchagua mechi zenye timu ambazo zenye uwezo unaokaribia na kulingana,kwa kuwa timu moja hupewa goli la kufikirika ambayo mara nyingi huwa ni ile dhaifu basi ni vyema kuchagua matokeo ya Suluhu huku ukiamini kuwa ile timu yenye nguvu zaidi huenda ikashinda kwa tofauti isiyozidi goli 1.Yaani 2-1 au 1-0 au hata 3-2. -FOURTYFIVE(45); hapa sasa ni mahala ambapo mechi za machaguo ya suluhu kuzingatiwa.Kutokana na mechi kuanza kwa suluhu ya bila kufungana,kuna uwezekano wa asilimia 80% ya hizo mechi kumaliza dakika 45 za kwanza bila kufungana ili uweze kuchagua suluhi ya dakika 45, inashauriwa kuchagua mechi ambazo zina upinzani mkubwa sana baina yao au mechi zenye timu zilizodhaifu sana. #7 . JIWEKEE KIASI KATIKA KU-BET. Huu mchezo unaathiri sana tabia-ya binadamu (Addictive).Kuna kipindi unasikia hamu ya kubet kila mara hata pale unapoona mkeka(Betting Form) umeharibika, ili tu uweze kurudisha kile kiasi cha pesa ulicholiwa.Hii hutokea kwa sababu ya kutojiwekea "kikomo". Weka kikomo ,mfano Tsh 5000/= tu itumike ndani ya saa 72.Itakufanya uwe na kikomo katika mchezo na kukusaidia kutopoteza kiasi kikubwa cha pesa kutoka mfukoni mwako. #8 . FUATILIA UTABIRI WA MITANDAONI. Ni vyema kufuatilia utabili wa mitandaoni kwa sababu huwa na takwimu sinazoonyesha historia, Perfomance, na matarajio ya mechi husika. Hakikisha una-zingatia mechi tano(5) zilizopita. -Head-to-head ya timu hizo. -Perfomance ya timu katika dakika 45 za kwanza -Majeruhi walio n'je ya kikosi kikuu. -Usajili waliofanya -zingatia idadi ya magoli ambayo timu hizo zinafunga(score) na kufungwa(concede). -zingatia idadi ya mechi ambazo timu imeshinda na kupoteza. -zingatia msimamo/stance ya timu katika mechi za nyumbani na ugenini. Kuna baadhi ya mitandao maarufu ambayo hutumika kutoa tabiri za mechi mbalimbali. (1)windrawin.com (2)predictZ.com (3)soccervista.com na (4)livescore.com tu kwa matokeo yaliyo "live" na ya mechi zilizopita.