Tuesday, October 11, 2016

Vidonda vya tumbo

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo. Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kama Helicobacter pylori. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-inflamatory Drugs kama Aspirin au Diclofenachuweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu. Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum. 💢Makundi ya PUD Kuna makundi makuu yafuatayo ya ugonjwa huu 1. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo(Gastric ulcers) 2. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers) 3. Vidonda vinavyotokea kwenye koo(Oesophageal ulcers) 4. Vidonda vijulikanavyo kama Merckel’s Diverticulum ulcers. 💢Visababishi vya PUD Vidonda vya tumbo husababishwa na 🔴Maambukizi ya bakteria aina yaHelicobacter pylori: Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yeyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 yaduodenal ulcers. Hali hii husababishwa zaidi na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili. Matokeo ya kushindwa huku husababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis), uambukizi ambao huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali. Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Parietal cells.Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wagastrin pia uharibika, na hivyo kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo. 🔴Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs:Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaaniprostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo. 🔴Uvutaji wa sigara: Uvutaji sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike tu kuwa uvutaji sigara pekee hausababishi vidonda vya tumbo. 🔴Vyakula au viungo vya chakula vyenye uchachu: Kinyume na dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama vile pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo. 🔴Watu walio katika kundi la damu la O:Imeonekana pia kwamba kundi la damu lijulikanalo kama blood group O, halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo. 🔴Unywaji wa pombe: Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. 🔴Vitu vingine: Vitu vinavyohusishwa na uongezaji wa madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na upasuaji wa tumbo(major abdominal surgeries), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo; na kubadilishwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini. 💢Dalili au viashiria vya PUD Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula. Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula. Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara.Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua.Kichefuchefu na kutapikaKupoteza hamu ya kula na kupungua uzitoKutapika damuKupata haja kubwa cha rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbaliUwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa za kupunguza maumivu (NSAIDs) kwa muda muda mrefu bila kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo. 🌟SULUHISHO KWA KUTUMIA VIRUTUBISHO VYA KIADA.🌟 🔶1) Aloe vera jel Hichi ni kinywaji kilochotengenezwa na mmea wa aloe vera na kama inavyofahamika, aloe vera inauwezo wa kutibu vidonda tofauti ikiwemo vidonda vya tumbo. Na kila aliyetumia ameleta majibu mazuri ya kuondoa kabisa vidonda vya tumbo. Inamanufaa mengi, manufaa mengine nimeongelea kwenye mada ya "Moyo". 🔶2) Bee Propolis Hii imetengenezwa na nta inayotolewa na nyuki wa asali, nta hii hutumika kukinga mzinga na bacteria wanaoweza kudhuru mzinga. Lakini pia nta hii ni muhimu sana katika miili ya binadamu. Manufaa hayo ni, 🔵ina ongeza kinga ya mwili 🔵ina saidia kuuwa bacteria hatarishi kwenye mfumo wa chakula. 🔵 Huondoa uchovu wa akili 🔵 inaongeza uwezo wa kupona 🔵 inapunguza mikonyanzi 🔵 inahusika na kutatua allergies.