Wednesday, September 14, 2016

UTAPIAMLO KWA WATOTO UNAEPUKIKA!!!!

UTAPIAMLO KWA WATOTO UNAEPUKIKA!

Je, wajua kwamba kwa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) asilimia 45 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinatokana na lishe duni?

Je, wajua kwamba watoto wa kundi hili wapatao milioni tano na laki 9 walifariki duniani mwaka 2015 pekee?

OKOA MAISHA YA MWANAO KWA KUMPATIA MLO KAMILI ULIOSHAMIRISHWA NA VIINI LISHE

SEMI MBALIMBALI TUNAZOZIISHI KATIKA JAMII

NI USEMI UPI UMEKUKAMATA?:

1. "Kuzaliwa masikini siyo kosa lako,ila kufa masikini ni ujinga wako." ~ Bill Gate

2. "Kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa." ~ Felix Bundala

3. "Heri kufa na mawazo yanayoishi, kuliko kuishi na Mawazo yaliyokufa." ~ Che Guevara

4. "Vita inamalizwa kwa vita na ili tuachane na matumizi ya bunduki inabidi itumike bunduki." ~ Mao ze Dong

5. "Sitamani kumjua babu yangu alikuwa nani, ninachotaka kumfahamu mjukuu wake atakuwa na tabia gani." ~ Martin Luther King

6. "Usimuulize mtu yoyote anayenijua mimi maana utamjua yeye kupitia mimi." Joe Lescot

7. "Muonekano siku zote hutengeneza uwezekano." ~ Lucky Crackent

8. "Hatuwapendi wanawake kwa sababu ni wazuri, ila tunawaona wazuri kwa sababu tunawapenda." ~ Luck Crackent

9. "Watu ni wengi ila binadamu ni wachache." ~ Fidel Castro

10. "Usiishi kwa sababu unaishi, tafuta sababu ya wewe kuishi." ~ Jay Ozil Cazorla Wilshere

11. "Hakuna mkate mgumu mbele ya chai." ~ Bob Sydou

12. "Kichwa kikubwa bila Akili ni Adhabu kwa miguu." ~ Thabiti Kube..

Lionel Andres Messi

HIV  NDIVYO  ILIVYO  , MGUU 1  WA  MESI  N  ZAID  YA  MIGUU 22  YA  WACHEZAJ  WA  CELTC : Lig  ya  mabngwa  baran  Ulaya  ilianza  rasmi  hapo  jana  kwa  michezo 7 ya  makundi A-D  huku  mechi  zngine 9  zkipgwa  leo  kuanzia  kundi  E-H , pa1 na  mchezo  wa  kiporo  wa  kundi  C kat  ya  Ct v/s Borusia  moncheng  gladbach . Ktk  mchezo  pekee  wa  kundi  C  kat  ya  FC BARCA v/s CELTC  mvua  ya  magol  iliwashukia  Celtc  ikiĆ“ngozwa  na  Brendan  Rodgers  Pa1  na  baadh  ya  majna  toka  EPL  kama , Kolo-2re ,  Adam  Amstong , Sinclair  na  Boyata , huku  mesi  akifunga  hat trick  ktk  mchezo  huo .  Mbali  na  hat trick  Mesi  amewaongoza  wachezaj  kutoka  AMERIKA  KUCN  toka  nchi  4  za  ARGENTNA , BRAZIL ,  URUGUAY na  CHILE  kufunga  gol 11 kat  ya  22  yaliofungwa  jana ,  huku  mengine 11  yakiongozwa  na  mjeruman  Joshua  Kimmich  kufungwa  na  wachezaj  wa  Ulaya  toka  mataifa  4  tofaut  ambayo  n  SPAIN , POLAND , SWITSLAND  na  GERMANY . Sasa  swali  je , Cr7  ata wakomboa  Celtc  leo?


Mwenyekiti wa bunge aomba radhi

Mwenyekiti wa Bunge amwomba radhi Mbowe
               

Hatua hiyo imefutia mwongozo ulioombwa na wabunge wawili Chadema, kuwa mchango wa Mbowe haukutambulika licha ya kufika Bukoba, kutoa misaada na kushirikiana na waathirika wa tukio hilo hadi sasa.

Aliyeanza kuomba mwongozo ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ambaye alihoji kwa nini mwenyekiti huyo wa Bunge amewatambua viongozi waliofika eneo la tukio na kutoa misaada lakini ameshindwa kumtambua Mbowe ambaye mpaka sasa yupo eneo la tukio na ametoa msaada.

Mbunge mwingine ni Pascal Haonga wa Mbozi ambaye alisema Mbowe ni kiongozi mkubwa na halitakuwa jambo la maana kama mchango wake hautatambulika kwani suala hilo siyo la kisiasa.

Kufuatia mwongozo huo, Zungu aliomba radhi na kuongeza kuwa anamtambua Mbowe kama kiongozi aliyetoa msaada kwa waathirika hao.

Awali, Mwenyekiti huyo wa Bunge baada ya kuingia ukumbini alitoa pole kwa waathirika wa tetemeko hilo lililoua watu 17 na kuwatambua watu waliochangia tukio hilo akiwamo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na wafanyabiashara.

 Baada ya kipindi cha maswali na majibu kuisha, mwenyekiti huyo aliwatambua wafanyabiashara wengine waliotoa msaada kwa waathirika hao lakini hakugusia msaada ulitolewa na Mbowe.