Monday, September 19, 2016

Ni muda upi sahihi kuingia kwenye mahusiano

Ninarudia tena (Zingatia hii ni Muhimu )

SOMO : NI MUDA UPI NI SAHIHI KWA MTU KUINGIA KWENYE MAHUSIANO MAPYA BAADA YA MAHUSIANO YALE YA KWANZA KUVUNJIKA.

●Watu wengi wanakurupuka na matokeo yake wanajikuta kila kukicha wanaumizwa kiasi kwamba hawana tena  hamu na mahusiano  tena, wamekata tamàa, hawaamini kama kuna mtu mwaminifu, hawataki kusikia habari za mahusiano, zaidi ya Yote hata kuna wengine walifanya maamuzi ya kuoa /kuolewa  si kwa sababu wanapenda ila kwa sababu ni umri tu umewatupa mkono hivyo wakaamua kudumbukia popote ila upendo hakuna, japo wameolewa ila moyoni hampendi aliye naye kwa 100%.Kwa hiyo yupo 50/50.

■NI MUDA GANI HASA UNATAKIWA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO MAPYA

1.Ni Muda ambao  una uhakika kuwa ,UKIMUWAZA EX ALIYE KUUMIZA, NDANI YAKO  HAUPATI UCHUNGU.

2.Ni Muda ambao  Umekwisha kutafakari kwa kina na kupata majibu  juu ya sababu zilizokufanya ulie kwenye uhusiano uliokuliza na Ex wako. Maàndiko yanasema siku ya mabaya utafakari. Tafakari usije ukarudia kosa lile lile.

3.Ni Muda ambao Moyoni Mwako hauoni kama kuna sababu ya kurudiana na Ex wako.Kama unaona bado unampenda usitafute mtu mwingine maana utamsumbua kwa sababu moyo wako hautakuwa   kwake bali kwa ex wako.

4.Ni Muda ambao Moyoni Mwako umemsamehe yule aliye kujeruhi na upo Tayari kumuacha aendelee na maisha yake pasipo kinyongo.

5.Ni Muda ambao mawazo yako hayapo Tayari kufanya maamuzi ya kutafuta mtu mwingine kwa nia ya kumkomoa ex wako, yaani kutaka kumkomeshea. Maana hapo ni kujiumiza mwenyewe na hayo ni maisha yako si ya ex wako.

6.Ni Muda ambao UMEMUOMBA MUNGU VYA KUTOSHA HADI MOYONI MWAKO UNAYO AMANI YA KRISTO

7.Ni Muda ambao UHUSIANO WAKO NA MUNGU HATA WEWE UKIJIKAGUA UNAONA KABISA UPO VIZURI SANA. Unajua Watu wengi mahusiano yao na wapenzi wao huwa yakivurugika hata mahusiano yao na MUNGU yanaharibika SANA.

8.Ni Muda ambao ukisikia habari za Ex wako haukasiriki na unaona hayo ndiyo maisha yake aliyoyachagua.

9.Ni Muda ambao umerelax na unautumia Muda wako mwingi kumtumikia MUNGU kwenye kusudi alilokuitia.

NB: VIGEZO HIVYO HAPO JUU NI DALILI NZURI KUWA SASA UPO TAYARI. UKIONA KUNA SEHEMU UNAKWAMA MUOMBE MUNGU AKUSAIDIE, NAYE ATAKUSAIDIA.

MUNGU AKUBARIKI

No comments:

Post a Comment